Konde Gang yasitisha Mkataba na wasanii wake Cheed na Killy.
Uongozi wa lebo ya Konde Music Worldwide (Konde Gang) inayo milikiwa na msanii Harmonize umetangaza rasmi kusitisha mkataba na wanamuziki wake Cheed na Killy kutokana na sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wao.
Imeelezwa. Lebo hiyo ambayo leo imetimiza miaka 4 tangu kuanzishwa kwake Oktoba 10, 2019, iliwasaini Cheed na Killy Septemba 2020 kwa pamoja kutoka lebo ya King’s Music ya mwanamuziki Alikiba.
Kwahiyo wamekaa miaka miwili chini ya lebo ya Konde Gang Wakati Konde Gang, Cheed na Killy kila mmoja amefanikiwa kuachia EP yake aliyomshirikisha Harmonize. Cheed alitoa “ENDLESS LOVE” na “THE GREEN LIGHT” ya Killy.
Huenda ikawa ni taarifa mbaya zaidi kwa mashabiki wa Cheed na Killy au hata wafuasi wa Konde Gang Worldwide Music.
No comments